RAY, UWOYA… WHY? KWA NINI KILA SIKU SKENDO?
Kwa nini majina yaleyale katika mistari hii? Ni kutokana na kile
kinachojiri. Kuna baadhi ya mastaa Bongo ni vigumu kukwepa kuwazungumzia
kutokana na drama zao za kila kukicha. Unaweza ukakwepa kuwazungumzia
Wema Sepetu, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Khaleed Mohamed ‘TID’
gazetini lakini wakawa wametawala kwenye mitandao ya kijamii. Kwa nini?
Ni kwa sababu hawakosi vitimbi. Kama siyo kufumwa wakifanya vitu vya ajabu, basi watakuwa wanagombana.
Kwa mara nyingine nazungumza nanyi waigizaji wa filamu za nyumbani, Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’ na Irene Pancras Uwoya.
Nianze na wewe Ray. Kama hukumbuki, nitakukumbusha. Alipofariki Steven Kanumba ‘The Great’, nilikuandika hapa. Nikakutahadharisha juu ya anguko lako katika sanaa kwa kuwa mshindani wako wa kibishara na swahiba wako Kanumba alikuwa ameondoka.
Sijui kama ulikubaliana na mtanzamo wangu kwa kuwa nilikueleza ni kwa jinsi gani kishindo cha anguko lako kitakavyokuwa kikubwa.
Wiki iliyopita Ray uligeuka gumzo. Kisa? Maadhimisho ya kumbukumbu ya marehemu Kanumba ya mwaka mmoja tangu alipoondoka kwenye uso wa dunia.
Sawa, ulifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kwenda ibadani Kimara, makaburini Kinondoni na katika Viwanja vya Leaders, Kinondoni, Dar.

0 commentaires:
Sema Tunakuskia na wewe