Diamond: Hakuna msanii anayenifikia kwa hela nayopata kwenye ringtones lakini

Suala la wasanii kunyonywa na makampuni ya simu kwenye mauzo ya ringtone
linamuuma kila msanii, hata Diamond ambaye ndiye msanii anayeingiza fedha nyingi
zaidi kuliko yeyote Tanzania katika biashara hiyo.

Jana kupitia Instagram, aliandika kilio chake:
Dah! hivi kweli Serikali imekosa majibu ya swali la mh: Mbunge kuhusu mapato ya
biashara ya ringtones..!? Kweli sasa naanza kuamini kuwa Serikali Inatukumbatiaga tu
kwa Mda mfupi na kututumia Wasanii kwenye Kampeni zao kwa Maslahi yao Binafsi,
kisha wanatudump baada ya kufanikiwa kwenye uchaguzi wao, bila kujali thamani na
Mmhango wetu kwao.
Hata hivyo kuna watu wanaoamini kuwa Diamond hapaswi kulalamika kwakuwa ndiye
msanii anayefaidi zaidi matunda ya muziki Tanzania.
Mmoja wa followers wake aitwaye Princestepp aliandika: Hupaswi kulaumu wewe

maanake kati ya wasanii wachache walioweza kula hela za watanzania chini ya ya
serikali ya rais wetu Kikwete ni wewe acha unafiki wasanii wengine ambao hawajapata
fursa kama yako walaumu vipi sasa?
Diamond alijibu: Mi nimekula pesa na bado nakula pesa kwa juhudi zangu za kujituma
jukwaani na kufanya show nzuri, sio kuwa naitwa kupewa pesa za ringtones nah!
Napewa show.... So nikiwa kama mfano mzuri kwa wasanii lazima niwe mstari wa
mbele kupigania haki za wasanii kiujumla.
Aliongeza, “Mi napigania haki zetu upande mwingine wananiona snitch.. wakati mi
naamini katika wasanii wote japo nadhulumiwa lakini hakuna hata anayefikia hela
nnayolipwa kwa rintones.. ila naona haiwezekani kwanini watufanye wajinga watu
wapewe haki zao.”

0 commentaires:

Sema Tunakuskia na wewe