DIAMOND NA NEY WA MITEGO WANYUKA SUTI NA KUCHEZA "POKER " KWENYE VIDEO YA MUZIKI GANI....

Pata picha mtu mzima Ney wa Mitego akiwa amepiga suti nyeusi na miwani yake kali ya rangi hiyo hiyo? Na pembeni yupo Diamond wakicheza poker kwenye casino na huku nyuma yao wakiwa wamezungukwa na watoto kadhaa warembo!! 

 Wasanii hao wataonekana kwenye video ya wimbo wao unaotikisa waves za radio kwa sasa, Muziki Gani, wakiwa kwenye muonekano nadhifu ndani ya suti. Video inafanywa na Adam Juma wa Visual La: Next Level bila shaka ikitoka itakuwa ni video nyingine ya kuzungumzwa mwaka huu. 
Kupitia Instagram, Diamond ameshare picha ya behind the scenes za video hiyo huku mpenzi wake Penny akiandika: “Maaaaaaamaaaa!!!my baby luks so elegant!!!! #proud of you, all the best baby #murderThatVideo.”

0 commentaires:

Sema Tunakuskia na wewe